September 27, 2018


Sitaki kumuongelea sana Rajabu Abdulkhali ‘Harmonize’ anayewakilisha Wasafi Classic Baby (WCB) aliyetoka kimuziki 2016 na Wimbo wa Aiyola kisha Bado uliomfanya kutengeneza ‘drama’ na Jacqueline Wolper Massawe ambayo ilizaa matunda kwa kiasi kikubwa.

Unaweza kuwa mgumu kuamini lakini, nyuma ya mafanikio ya Harmonize, Wolper kahusika kwa asilimia zake kwani drama yao ilizaa nyimbo kadhaa zikiwemo Sina, Niambie na mwisho akamalizia Nishachoka kisha akahamia kwa Sarah ‘Mzungu’.

Kuna msemo usemao; maji hufuata mkondo na mazoea hujenga tabia! Tumekuwa tukiona kiki za aina mbalimbali zikitokea ndani ya Lebo ya WCB, mfano, Rayvanny kuachana na mzazi mwenziye, Fahma kisha ukaachiwa wimbo wake wa Siri, Rich Mavoko kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na Lulu Diva na baada ya muda ukaachiwa wimbo wake wa Rudi akimshirikisha Patoranking kutoka Nigeria.

Nyuma ya pazia, anayeongoza kwa kiki hizo ni bosi wao kutoka WCB ‘Diamond Platnumz’, ukiangalia kalenda ya mwaka, kwa miaka minne mfululizo amekuwa akifanya hivyo kama siyo kuwataja warembo kwenye nyimbo zake, kuwatumia kwenye video zake basi lazima atatengeneza kitu kupitia warembo hao ili ‘kubusti’ nyimbo zake.

Kiki hizo mara nyingi zimekuwa zikiwa-shtua mash-abiki na kuwa-fanya kwa siku kadhaa wakibaki kumzun-gumzia kwa muda mrefu huku wengine wakimponda kwa kum-uona hana maa-na.

THIS IS TOO MUCH!

Ndivyo unavy-oweza kusema kwa lugha nyepesi! Mashabiki wamezi-choka kiki anazofanya Diamond tangu ameanza kufanikiwa kimuziki hadi alipo. Hizi ni baadhi ya kiki za warembo alizowahi kutoka nazo;

WEMA SEPETU

Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006, amehusika kwa kiasi kikubwa kumpandisha Diamond katika Muziki wa Bongo Fleva.

Diamond alishawahi kumtumia Wema kama video queen kwenye wimbo wa Moyo Wangu. Drama za wawili hao za mara kwa mara zilimfanya Diamond kumuimba Wema kwenye wimbo wake wa Nimpende Nani pale alipochombeza kwa kusema; Na Utuache tulale.

Kama haitoshi akamtaja hadi mama yake Wema kwenye Wimbo wa Kesho akamalizia kumtaja kwenye wimbo wake wa Sikomi kwa kuelezea historia yao ya mapenzi. Kuonesha kuwa amekuwa akimtumia Wema kutengeneza kiki, Diamond alifanya hivyo tena wakati wa utambulisho wa msanii wake, Maromboso ‘Mbosso’ katika Hoteli ya Hyatt Regency.


Katika usiku huo, Rayvanny alimaliza shoo yake na kumuita jukwaani Wema na baada ya kupanda naye akamuita Diamond ili afanye makamuzi. Kumbuka katika kipindi hicho hawakuwahi kuwa karibu kwa zaidi ya mwaka.

HAMISA MOBETO

Ukichunguza kwa undani unaambiwa Hamisa ndiye wa kwanza kutoka na Diamond kabla ya Wema. Najua unaweza usiamini hili! Sikia;Mwanamitindo huyo maarufu ambaye pia ni mjasiriamali na msanii wa Bongo Fleva, ametawala kwenye Video ya Salome iliyozaa matunda ya mtoto aliyezaa na Diamond aitwaye Dylan.

Panda shuka za wawili hawa ziliendelea baada ya kiki ya kumlea mtoto wao na kufikishana mahakamani. Ghafla Diamond akaingia studio na kutoka na ‘Niache’. Umeshawahi kuyatafakari mashairi ya wimbo huo? Unaweza kudhani Diamond hatakaa na kuzungumza tena na Hamisa.


Wiki kadhaa mbele kabla ya kuachia wimbo wake wa African Beauty, ikasambaa video ikiwaonesha akiwa chumbani kimahaba na Hamisa.

ZARINNAH HASSAN ‘ZARI’

Diamond alianza kumtumia Zari aliyezaa naye watoto wawili, Nillan na Tiffah katika video ya Utanipenda akiwa kama video queen. Licha ya kuachana Ferbuari, mwaka huu na kubaki kama walezi wa watoto wao, Diamond amekuwa akiendelea kumtumia Zari katika kutengeneza kiki za nyimbo zake.

Drama ilianza kwa meneja wa Diamond, Babu Tale kwa kutupia picha katika Mtandao wa Instagram akienda Afrika Kusini kwenye makazi ya Zari huku akisema anaenda kusuruhisha ugomvi wa wiwili hao. Baada ya muda akasema alikuwa ameenda huko kuzungumzia kuhusu matunzo ya watoto wao.

Drama ziliendelea baada ya Zari kupokea zawadi za pafyumu kutoka kwa Diamond na kumshukuru katika Mtandao wa Snapchat. Kumbuka haya yote yalikuja kwa sababu ya Wimbo wa Iyena aliokuwa akiandaa kuutoa ambao ndani yake alionekana akimuoa Zari.

USHAURI

Diamond ni msanii mkubwa ambaye bila kutegemea kiki au kuwatumia warembo aliowahi kutoka nao anaweza kusimama vizuri tu.

Hadi alipofika, ameweza kujiwekea heshima kubwa ndani na nje ya nchi kupitia nyimbo zake hivyo ni wakati wa kujiamini kwa kile anachokifanya na kuiga mifano ya wasanii wakubwa waliomtangulia.

Hebu tumwangalie msanii mkongwe kama Jaydee. Ni lini Jaydee amekuwa na skendo? Lakini je, amewahi kushuka kimuziki mpaka sasa? Jaydee siku zote haandikwi kwa skendo bali habari ambazo zinatokana na kinachoendelea katika maisha yake. Waulize AY, FA, Sugu, Profesa Jay, ni lini walitegemea kiki katika muziki wao?


Bado naamini kufanya kolabo na wasanii wengine wa ndani na nje ya nchi kunaweza kumpandisha msanii zaidi, kwa hiyo Diamond aendelee kuamini kolabo za nje kama alivyofanikiwa kwa My Number One Remix akiwa na Davido, Kidogo akiwa na P Spuare, Nana akiwa na Mr. Flavour, Fire akiwa na Tiwa Savage wote hao wa Nigeria.

Kutoka Global Publishers

3 COMMENTS:

  1. binafsi km sioni kuwa ni tatizo sababu hizo ni life style za mtu hasa wasanii kwani ata wa nje nao wana aina zao za kiki, tumeshashuhudia wakati flan jayz zilitokea habari wameachaba na beyonce kumbe ilikuwa ktk harakati za kutangaza tour yao flan hivi, kanye west na kim pia ilikuwa hivyo. kwa hiyo cyo issue kubwa ambayo inawdza kukuumiza au kumuumiza mtu eti kwanini diamond daily anakuja na hizi kiki.

    ReplyDelete
  2. kila mtu anastaili yake ya kufanya biashara, hata ww hapo leo umeona uandike habari za Diamond ili kuvuta Tension ya wasomaji

    ReplyDelete
  3. Huko sasa ni kumuingilia msanii kwenye kazi zake na mikakati yake ya kuuza kazi zake. Muhimu ni kusimamia na kuzingatia maadili, sioni ubaya wa Diamond kufanya anachopendezewa nacho. Hata hao warembo anaowaimbia hawana tatizo na hilo vinginevyo wangeshamlalamikia hata kumshitaki. Siku zote usidhani wewe ndie uwe mshauri mkubwa wa kila fani, hapana. Kwenye fani hii ya muziki ni wazi Diamond hahitaji kushauriwa na gazeti hili juu ya nini aimbe na nini asiimbe kumuingilia huko ndiko sasa kutakuwa TOO MUCH.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic