September 4, 2018

6 COMMENTS:

  1. Sio kosa kusema kwamba baada ya kun'gatuka Mualimu Nyerere kutoka madarakani basi kiongozi sahihi wa kumrithi angepaswa kuwa Magufuli au mtu mwenye maamuzi ya kimagufuli pengine Tanzania tungekuwa tupo mbali sana kimaendeleo. Ni maoni yangu binafsi na simaanishi kwamba waliomtangulia hawakufanya kitu lahasha bali Magufuli ameleta kitu tofauti katika uongozi wake kinyume na mazoea ya kitanzania ya kuoneana aibu katika uwajibikaji.
    Bara la Africa ni bara asirika kutokana na kutawalia kwa mabavu na kiakili za wazungu kwa miaka mingi. Wazungu waliibia Africa hakuna walichoacha kuanzia madini,wanyama hadi binaadamu.Tunaposema watu ni utajiri yaani rasilimali watu kama si biashara ya utumwa iliowahamisha mamilioni ya waafrica waliotapakaa Dunia nzima basi Africa ndio ingekuwa bara linaloongoza kwa watu duniani na siku zote penye watu pana mengi ndio maana wamerakani walipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe na zaidi ya watu laki tatu au zaidi kupoteza maisha ili kuunganisha nguvu za watu wao kuwa kitu kimoja lakini cha msingi ya vita yao ilikuwa ni vita ya kupigania rasilimali watu na walishinda vizuri vita hiyo leo tunapoizungumzia Marekani tunazungumzia Taifa moja,nchi moja yenye idadi ya watu zaidi ya milioni mia tatu na ni super power. Mchina kwa kutambua umuhimu wa rasilimali watu katika maendeleo ya nchi haraka haraka wakafanya mapinduzi ya kimaajabu ya kiuchumi kiasi kumnyima uzingizi Marekani na China hivi sasa miongoni mwa super power mtarajiwa. Na katika vita hiyo hiyo ya kupigania rasilimali watu ndio iliyopelekea kuanguka kwa taifa la kisovieti la USSR la kirusi kutoka super power wa dunia hadi kuwa taifa la kawaida hasa kiuchumi baada ya nchi nyengine kumeguka kutoka katika Muungano wa kisovieti. Sasa inasemekana nchi yenye idadi kubwa zaidu ya watu weusi duniani ni Brazil ikifuatiwa na Nigeria au Marekani,nchi kama Trinidad and Tobago,Belize,Haiti,Jamaica yaani kule carerebian kote ni watu weusi pamoja na maeneo mengine hasa visiwa vinavyozunguka pwani ya Australia na Indonesia watu weusi utawakuta wametapakaa na sababu kubwa ya watu weusi hao kuishia katika nchi hizo kinyume yakuwepo hapa Africa,hawakupelekwa kule kwa ajili ya matembezi au vacation lahasha,walipelekwa kule kama vitendea kazi kama watumwa. Africa kwa miaka mingi baada ya rasilimali watu yake kuporwa bara la Africa lilibakia kama njiwa alienyofolewa mabawa.Bara Africa la lilishindwa kukabiliana au kujidifend kutoka kwa wavamizi wa nje baada ya watemi hao wa nje kutamkiwa na biashara ya utumwa na kuamua kuja kuweka makazi yao kibabe Africa. Kwa vyovyote vile Africa iliathiriwa sana na biashara ya utumwa. Bila ya utumwa hapana shaka Africa ingekuwa miongoni mwa mabara imara zaidi kiuchumi duniani kama si super power kwa sasa. Kama waafrica lazima tujuwe nini na nani na wanaoendelea kutukwamisha hadi kufikia hapa tulipo. Tukirudi kwa Magufuli baada ya Nyerere kupigana kufa kuhakikisha Africa inakomboka kutoka kwa wavamizi ilikuwa lazima apatikane mkombozi mwengine wa kweli asiekuwa na huruma kupambana na mvamizi mwengine hatari zaidi amabe ni umasikini. Kiuhalisia umasikini wa muafrica upo katika akili yake yaani waafrica ni masikini wa akili zaidi kuliko mali na tunweza kusema bado ni muendelezo wa fikra mgando za kutawaliwa kutoka kwa wakoloni.Na ndipo ninapomvulia kofia Magufuli kwani kama utamfuatilia katika mahubiri yake anachokifanya hivi sasa ni kuwatoa watanzania kutoka katika fikra mgando za haiwezekani na kuwapeleka katika fikra endelevu za tunaweza ni somo la saiokolojia sahihi kabisa analorejea mara kwa mara kwa watanzania. Kubwa zaidi kwa Magufuli ni uadilifu wa asilimia mia moja 100% katika kuwatumikia wananchi wake na kuwa makini katika kuliepusha Taifa na wananchi wake kutegemea misaada ya kigeni pamoja na kuwa na zero tolerance katika kupambana na ufisadi kutomuunga mkono ni sawa na uhaini.

    ReplyDelete
  2. Hahaha kweli ww unamawazo finyu nn amekifanya makufili zaidi ya kuitia nchi umaskini wtu wote hohi hahe taabani halizao

    ReplyDelete
  3. Mpendwa mchukie Magufuli kiboko. Anaeuliza kafanya nini Magufuli atakuwa ana tope za chooni kwenye ubongo wake.

    ReplyDelete
  4. Tena inabidi kuogopwa kama ukoma, maisha ya sasa ni sawa maana wengine tulitoka jasho wakati wengine walikuwa wanaagiza na kupata bila kutoka jasho, wewe bado huoni Magufuli kaleta usawa? Tuache chuki za kinafiki, tuone ukweli na kumuombea alete mageuzi yake tunayoyataka. Ulipenda watu walivyokuwa wanalewa muda wa kazi na wakati wote watu wapo kwenye pool na mabao bila ya kufanya kazi? Jamani tuzungumze ukweli tuache longolongo Tanzania ni ya kwetu na anachofanya kwa ajili ya watanzania.

    ReplyDelete
  5. Sina shaka kuhusu maendeleo ya nchi, hususa ni kiuchumi. But nina wasiawasi na mwelekeo Wa demokrasia yetu.
    Ni jukumu letu kama watanzania wenye uchungu na Taifa letu. Kipi tunakihitaji kwanza, DEMOCRACY or MAENDELEO.
    Nchi nyingi ambazo zmeendelea ukisoma historia zilianza kuua demokrasia kwanza. After kufikia level nzuri ya kimaendeleo ndio ikarudisha demokrasia.

    ReplyDelete
  6. Demokrasia hiyo imekuwa miaka yote na tumeendelea kuwa wanyonge kwa ajili ya hilo, hebu tuone mwelekeo kwa pamoja, kwa sababu anachofanya siyo kigeni sana ila kwa sababu mtazamo wa miaka mingi umekuwa mgumu kufikiwa ndo maana tunaona kama kitu kigeni kabisa. Huu ni mwaka wa tatu tu, hebu tuone mwaka wa nne tutakuwa wapi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic