September 21, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umewasamehe wachezaji wake watatu Said Makapu, Mwinyi Haji na Pius Buswita ambao hawakuwa sehemu ya mchezo uliopita dhidi ya Stand United.

Wachezaji hao waliondolewa kambini na Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kwa utovu wa nidhamu na sasa watakuwa sehemu ya kikosi kuelekea mechi zijazo za Ligi Kuu Bara

Uongozi umesema wachezaji hao wameomba radhi kwa Kocha wao ambaye ameonekana kuwa mbogo kwa wale wote wanaoleta UFADHA ndani ya timu bila sababu za msingi.

Wachezaj hao watatu sasa watakuwa sehemu ya kikosi ambacho kitacheza na Singida United Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Yanga itashuka Taifa majira ya saa 1 za usiku ambapo mechi hiyo dhidi ya Singida itaruka mubashara kupitia kituo cha Azam TV.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic