September 4, 2018


Kiungo mpya wa klabu ya Yanga, Mohamed Issa Banka, amefungiwa kucheza soka na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa muda mwaka mmoja.

Banka amefungiwa kwa kosa la kufeli kwa vipimo ambavyo viliendeshwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) katika michuano ya CECAFA Challenge Cup, iliyofanyika mwaka jana nchini Kenya.

Taarifa zimesema kuwa timu ya Zanzibar na klabu ya Mtibwa walipewa majibu kuhusu vipimo hivyo ndiyo maana klabu ya Mtibwa Sugar haikuweza kumtumia kiungo huyo tangu Februari 2018.

Wakati huo Yanga ilifanikiwa kumsajili Banka bila kujua kama amefungiwa mwaka mmoja na CAF.

Wakati taarifa hizi hazijatoka, hivi karibuni uongozi wa Yanga ulisema kuwa Banka yupo kwao Zanzibar akiiguza majereha ya goti na ikitajwa kuwa sababu ya kuendelea kukosekana kwenye kikosi cha Yanga.

4 COMMENTS:

  1. Safi saaana eti wao ndio wanajua skauting wakati wa usajili na ndio mabingwa wa kuingiza mkenge timu nyingine katika usajili..ndege mjanja amenasa tundu bovu��������

    ReplyDelete
  2. Sasa si Skauting imefanyika? Ujinga wake nini?

    ReplyDelete
  3. TARIMBA hawakumshirikisha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic