YANGA YAWAPA ONYO SIMBA
Baada wa wadau na baadhi ya mashabiki wa klabu ya Simba kuanza kuhoji juu ya ratiba iliyorekebishwa, uongozi wa Yanga umewataka kufunga mdomo kwa sababu hawajaipanga wenyewe.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema kuwa ratiba hiyo hawajapanga wao hivyo hakuna haja ya watani zao Simba kuanza kulalama bila sababu za msingi.
Ten amesema kuwa hakuna anayepaswa kuanza kuwatumia lawama kwa maana hawahusiki hata kidogo na badala yake ni vema zikapelekwa Bodi ya Ligi ambao ndiyo wapangaji.
Hatua hiyo ya Ten kulitolea ufafanuzi limekuja mara baada ya wapenzi na baadhi ya mashabiki wa Simba kuanza kusema kuwa Yanga wamependelewa.
Katika ratiba hiyo iliyofanyiwa marekebisho baada ya kusimama kwa muda kupisha mechi za kitaifa, inaonesha Yanga itacheza mechi 11 mfululizo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sawa na baadae ysnga zitaelemewa na mechi mfululizo ugenini na huku mnyama akibakia nyumbani pia mfululizo
ReplyDeleteHuyu msemaji kihiyo kweli kweli. Nani kawalaumu Yanga?Watu wamelalamikia ratiba iliyopangwa ba Bodi ya ligi. Na sababu kubwa ni TFF kutaka Yanga ipate mapato ya kuwezesha kulipa deni la TFF. Kwani timu mwenyeji inachukua mapato yote msimu huu na ndio sababu ya kubadili ratiba.Kapigwa punda wa nyuma Yanga punda wa mbele ndio anayelia.AJABU SANA.
ReplyDeletepovu litawatoka sana.....nyie si ndo mliosema yanga hakuna kupendelewa tena kwakuwa malinzi(yanga) katoka na kaingia karia(simba).....sasa vipi tena,malinzi karudi tff au karia kawa yanga?
DeleteHakuna anyeilaumu Yanga kwa kupangiwa hivyo kama ni lawama basi TFF nido wanaolengwa, ajabu msemaji wa Yanga kuona tofauti na ukweli huo.
ReplyDeleteUpuuzi mbona kabla ya ligi kuanza Zahera alilalamika kwa nini simba wanaanza mechi tatu nyumbani wakati wao ugenini.ni simba aliyeppanga ratiba
ReplyDeletemtasema sana hao ndo jangwani.
ReplyDelete