September 4, 2018



Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta anayecheza katika klabu ya KRC Genk ya Belgium na mshambuliaji wa Al Hilal ya Sudan Thomas Ulimwengu wametua nchini leo alfajiri kujiunga na kambi ya timu hiyo inayojiandaa kuivaa Uganda wikiendi hii jijini Kampala.

Stars inajiandaa na mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon dhidi ya Uganda, mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka wa Tanzania na Uganda.

Wachezaji wengine wanaokipiga nje ya Tanzania ambao wamejiunga na kambi hiyo ni pamoja na Rashid Mandawa anayekipiga nchini Botswana na Ramadhani Kessy anayetokea nchini Zambia.

2 COMMENTS:

  1. Kina Samatta wamewasili leo lakini wiki iliyopita kuna wachezaji kocha kawatimua kwasababu wamecherewa kwa masaa kuripoti kambini. Tunajimaliza wenyewe.

    ReplyDelete
  2. Kocha hajui soka la bongo, msameheni bure. Atawaita tu siku moja.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic