September 4, 2018







Kumekuwa na taarifa kuwa uongozi wa Yanga unavutiwa na beki Rwabutaye Abdoul kutoka Rayon Sports.

Lakini mmoja wa viongozi wa Yanga amesema kuna mchezaji wa Rayon ambaye wanaamini atawasaidia baadaye na Abdoul ndiye amekuwa wakimtumia kumpata mchezaji huyo.

“Ni kweli Abdoul ni mchezaji mzuri lakini ana mkataba na Rayon, sisi tunachofanya ni kupambana kumpata mchezaji mwingine wakati wa dirisha dogo.

“Abdoul atakuwa anatusaidia, mara atakapomaliza mkataba basi tutapambana kumnasa. Lakini nafikiri wengi hawajaelewa, wanadhani tunamtaka Abdoul,” alisema.

Kulikuwa na mgogoro mkubwa wakati beki huyo akitua Rayon kutoka APR na klabu hizo mbili ni wapinzani wakubwa.


Lakini wakati Yanga wakisema hawana mpango na Abdoul, tayari uongozi wa Rayon Sports umesisitiza, beki huyo Mnyarwanda ana mkataba.

Katika tofuti ya Rayon Sports, imeonyesha klabu yoyote inayotaka kumnasa Abdoul au mchezaji mwingine wa Rayon mwenye mkataba, itakuwa matatizoni.

Rayon Sports imesonga mbele katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ikiwa na USM Alger ya Algeria huku Yanga na Gor Mahia zikiondolewa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic