September 3, 2018


Kikosi cha timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes' kimeendelea na mazoezi huko Kampala ya kujifua kuelekea mechi dhidi ya Taifa Stars.

Uganda watakuwa wanaikaribisha Stars kucheza mechi hiyo itakayopigwa Septemba 8 jijini Kampala.

Kueleka mechi hiyo, straika hatari wa Simba, Emmanuel Okwi ameonekana akijifua vilivyo kwa ajili ya kukipiga na Stars.

Okwi alikuwa majeruhi na ilipelekea akakosa mechi mbili za mwanzo katika kikosi chake cha Simba lakini sasa hali yake inazidi kuimarika.

Uwezekano mkubwa wa Okwi kucheza mechi dhidi ya Stars upo kutokana na mwenendo wake mazoezini kuonesha hali yake kuwa fiti.

2 COMMENTS:

  1. Kweli wachezaji wa kwetu hawajitambui. Huyu jamaa inasemekana ni majuruhi na bado amewahi kambini kwenye timu yao ya Taifa. Wale wa hapa wamechelewa. Sasa tumngoje kama baada ya mechi ya timu ya Taifa atawahi kujiunga na klabu yake.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Lazima atachelewa kujiunga na klabu yake baada ya mechi ya uganda cranes. Hata niyonzima atachelewa.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic