UONGOZI YANGA WATAJA UTOFAUTI WA KIKOSI CHA SASA NA MSIMU ULIOPITA
Wakati kikosi cha Yanga kikiwa tayari kushuka dimbani taifa leo kukipiga na Stand United, uongozi wa klabu hiyo umesema aina ya wachezaji walionao kwa sasa hawana utofauti zaidi na wa msimu uliopita.
kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili pamoja Kamati ya Mashindani, Hussein Nyika, amesema kikosi chao kina mchanganyiko wa wachezaji wenye uazoefu na vijana.
Nyika ameeleza kuwa Yanga ya sasa na msimu uliopita haina utofauti mkubwa kiasi cha kwamba inaweza ikatofautishwa bali wachezaji waliopo ni wale wakongwe pamoja na vijana.
"Kikosi ni kilekile, hakuna utofauti zaidi na msimu uliopita kwa maana tuna wachezaji vijana na wakongwe ambao wamekuwa wakishirikiana kwa namna moja ama nyingine kuisaidia timu kupata matokeo uwanjani" alisema.
Yanga inashuka Uwanja wa taifa majira ya saa 12 jioni kukipiga na Stand United ambao tayari wana siku kadhaa hapa Dar es Salaam kusubiria mechi hiyo.








0 COMMENTS:
Post a Comment