September 2, 2018


Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga ameonesha dhamira ya kuutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kutaka kushinda mechi 10 mfululizo, imeelezwa.

Zahera amefunguka na kusema kwa sasa nguvu zote anazielekeza katika kuwaandaa vijana wake ili kuhakikisha wanaanza vema zaidi baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kocha huyo ameeleza malengo yao ni kuhakikisha wanapata alama 30 ikiwemo zile za Simba watakapokutana Septemba 30 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mkongomani huyo ana imani kubwa ya kikosi chake kuimarika kutokana na upinzani walioupata kutoka kwenye mashindano ya kimataifa baada ya kucheza na vigogo kama USM Alger na Gor Mahia FC ya Kenya.

Kwa sasa kikosi cha Yanga kimezidi kujifua kwa ajili ya mechi za ligi kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi jijini Dar es Salaam.

3 COMMENTS:

  1. Pole sana kocha ni siku ambayo utafungashiwa virago

    ReplyDelete
  2. Tunakupa hongera toka leo kwa ubingwa hasa kama ulivotamka kuwa Simba hawana uzalendo kwa kuchelewa kwao kuripoti kambi ya kikosi cha timu ya taifa. Toka ufike
    umefanikiwa kukifanya kikosi chako cha yanga kuwa chenye hali yajuu kinidhamu. Wachezaji wako
    wamekuwa wenye nidhamu ya hali ya juu na wenye uzalendo hawajawahi hata mara moja kuingia ndani ya migomo au kususa mazoezi ijapokuwa hawakuwa wanalipwa mishahara lakini uzalendo mbele. Ile kufungwa katika mechi za kitaifa ilikuwa bahati mbaya hasa ile ya mwisho kule Ruwanda kwakuwa kulikuwa na mvuwa na kiwanja kujaa maji. Wacha kufuzu mechi kumi zote za nyumbani pamoja na ile ya Simba na kujikusanyia pointi 30, tunahakika utafuzu mechi zako zote za musimu na mfungaji bora kuwa Ajib na yule mpya mwenye kiwango cha ajabu. Hongera tokea sasa kwa ubingwa.


    ReplyDelete
  3. Kocha gani wa mitandaoni? Kila kukicha haachi kujitapa kuwa kocha mwenye uwezo. Anajitapa kuwa wachezaji wa Congo wanauzalendo na nidhamu yaani hovyo kabisa.Ninachokiamini Mimi kama wachezaji wa Congo wangekuwa na nidhamu na uzalendo basi hakuna nchi ya kuogopwa Africa kisoka kama Congo.wachezaji wao wametapakaa katika nchi za Ulaya na kuchukua uraia kule na kugoma kuichezea nchi yao ya asili kama wanavyofanaya wachezaji wa mataifa mengine.Huyu kocha anatakiwa kuacha kufanya kazi kwa mdomo na badala yake achie vitendo vyake viongee aige kwa mzungu wa SIMBA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic