September 2, 2018


Watu wawili wamefariki na wengine wawili kujeruhiwa usiku wa kuamkia leo huko Dunga, Zanzibar, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kushika moto.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema gari hilo aina ya Toyota IST lililokuwa likitokea Kiwengwa, lililipuka baada ya tenki lake la mafuta kuvuja kufuatia kugongwa na jiwe.

Majina ya waliofariki na kujeruhiwa yalikuwa hayajapatikana hadi tunakwenda mitamboni.  Hata hivyo, tutawajuza wasomaji wetu mara tu tukipata habari zaidi kuhusu tukio hilo.

Picha na Global Publishers.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic