Kiungo mshambuliaji wa timu ya Yanga, Ibrahim Ajibu ameomba kujitoa kwenye kikosi cha kwanza leo kitakachocheza dhidi ya KMC katika Uwanja wa Taifa ili aweze kupumzika.
Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema, Ajibu ameomba kujitoa kwenye kikosi kwa kocha Mkuu Mwinyi Zahera hivyo hatakuwa ndani ya kikosi kitakachocheza.
"Ajibu ameomba kutocheza leo kwa kuwa anasumbuliwa na maumivu ya mgongo aliyapata katika mchezo uliopita dhidi ya Alliance, mwalimu amemruhusu hivyo atatumia wachezaji wengine kuchukua nafasi yake leo," alisema.
Ajibu amekuwa na mchango mkubwa ndani ya timu katika michezo saba ambayo wamecheza kwa kuwa amehusika kwenye jumla ya mabao 11 kati ya 14 ambayo Yanga wameshinda na kuifanya timu kuwa na point 19.
0 COMMENTS:
Post a Comment