Kocha Mkuu wa Alliance, Mbwana Makata amesema kilichomfanya ajing'oe kwenye benchi la ufundi wakati timu yake ikifungwa mabao 5-1 dhidi ya Simba jana ni kutokana na kuingiliwa maamuzi.
Kabla ya mchezo Alliance walifanya mabadiliko ya mlinda mlango Said Lubawa nafasi yake ikachukuliwa na Kelvin Richard kwa kilichodaiwa ni sababu ya kiufundi.
"Benchi la ufundi limekuwa likiingilia mipango katika kazi yangu, kikubwa kwenye mechi ya jana tulikuwa tumepanga kikosi cha kuiua Simba, uongozi ukaingilia na kupanga kikosi, nimeamua niwaachie viongozi wafanye kazi," alisema.
Alliance FC wamecheza michezo 11 na kufanikiwa kukusanya pointi 5 wanaburuza mkia kwenye msimamo kwenye ligi Kuu Bara.
Mimevutiwa sana uwezo wa Saidi khamisi Ndemla hasa kunako upigaji wa pasi ingawa bado anatakiwa kupambana zaidi kuongeza kasi katika suala la (hustling) yaani kuwa mwepesi na haraka zaidi kwenye kunyanganya mipira na kuitawanya mahala husika kwa kasi zaidi, kama atamungalia Ngolo kante kwa umakini anavyofanya kazi basi atanielewa ninachojaribu kukieleza. Najua Ndemla kiasilia ni kiungo mshambuliaji zaidi kuliko kiungo mzuiaji lakini kocha amempa bahati ya kuonesha uwezo wake na kwa kiasi fulani amecheza vizuri asibweteke aongeze bidii kwani uwezo anao kuliko wachezaji wengi wanaotajwatajwa kila mara. Ndemla ni moja ya vijana hazina kwa kizazi cha sasa hana muda wa kusubiri tena lazima aoneshe uwezo wake sasa ni vita binafsi ili kuyatawala mazingira yake ya kazi kama ilivyo wachezeji wengine na atakae zembea basi ndie atakaekubali kuwa daraja la watu wapite wakienda juu yeye abakia pale pale. Katika kazi mfanya kazi mwenye ujuzi wa nafasi za aina tofauti za kazi ndio muhimu na si rahisi kukosa kazi. Wapo viungo kweli taifa stars lakini kama Ndemla atakaza basi atakuwa msaada mkubwa kwa timu ya Taifa kutokana na uwezo wake kupiga zinazowafikia walengwa mia kwa mia 100% na kwa aina ya washambuliaji tulionao kama Samata basi uwepo wa Ndemla aliekamilika ingekuwa sawa na chai iliyoongezewa tangawizi.
ReplyDeleteHebu jifunze kuwa unaandika ukweli..mwenyewe umeandika eti uongozi uaingilia maamuzi ya kocha..Kilichomng’oa kocha ni uongozi wa Alliance na sio Simba kama kichwa chako cha habari kinavyosema. Hapo msomaji akisona kichwa cha habari anataka kujua ni namna gani Simba imemuondoa kocha..akifungua anakuta kitu tofauti wala simba hausiki.acha kutuchezea akili na hii tabia yako!
ReplyDelete