October 25, 2018


Uongozi wa Simba umebainisha kuwa umakini wa kamati ya usajili umesaidia kuweza kumnasa kiungo mkabaji, Cleoutus Chota Chama, "Triple C" ambaye amekuwa msaada ndani ya timu.

Chama raia wa Zambia, amefanikiwa kufunga mabao mawili msimu huu na ametoa pasi moja ya bao hali inayomfanya azidi kukubalika kwa mashabiki kutokana na uwezo wake .

Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema kazi ya kumleta Triple C ilikuwa chini ya aliyekuwa akikaimu Uenyekiti Kamati ya Usajili ya Simba.

"Aliye nyuma ya Usajili wa Chama ni Cresentius Magori,  aliyekuwa akikaimu Uenyekiti Kamati ya Usajili ya Simba na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu, mnazikumbuka sarakasi za wazambia hadi FIFA ? basi aliyekuwa nyuma ni Magori katuletea Chama Kiungo Sukari," alisema.


2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic