October 16, 2018




Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike amesema wako tayari kwa mechi ya leo dhidi ya Cape Verde. Mechi hiyo itarushwa moja kwa moja na Azam Tv.

Amunike amesema wameyafanyia kazi makosa yao yaliyotokea katika mechi ya kwanza na kusababisha kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao 3-0.

“Tumepata muda wa kuyafanyia kazi makosa yetu, tunaamini leo hakuna mjadala zaidi ya pointi tatu. Haitakuwa kazi nyepesi lakini tutapambana,” alisema.

Pamoja na marekebisho yaliyofanyika ikiwemo kumuongeza kiungo Erasto Nyoni kutoka Simba, Amunike amesema vijana wake wako katika morali ya juu kabisa.

Mechi hiyo itapigwa saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic