October 16, 2018



Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Zacharia Hans Poppe atafikishwa mahakamani leo kujibu kesi inayomkabili ya kugushi nyaraka na utakatishaji wa fedha.


Hans Poppe amerejea nchini na kujisalimisha kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


Hans Poppe ataunganishwa kwenye kesi ya kugushi nyaraka na utakatishaji inayowakabiri Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.

Ndugu yake wa karibu amesema Hans Poppe aliamua kurejea baada ya matibabu.


"Amerejea akijua atakamatwa, ukisema amejisalimisha kwa lengo la kuona kesi inasikilizwa kwa kuwa anaamini hana tatizo," alisema ndugu yake wa karibu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic