Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema wamekuwa wakiyafanyia kazi masuala kadhaa kuhakikisha wanakuwa bora.
Aussems raia wa Ubelgiji, amesema moja ya suala wanalolifanyia kazi ni kutumia nafasi wanazozipata.
“Tunatengeneza nafasi nyingi sana lakini tumekuwa hatufungi, hivyo tunalazimika kufanya kazi ya ziada.
“Lazima tuhakikishe makosa yanapungua ili kutengeneza uhakika wa mambo kwa kuwa tunatakiwa kufunga,” alisema.
Kikosi cha Simba kimekuwa kikiendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani kuendelea na maandalizi ya ligi ingawa inawakosa wachezaji kadhaa ambao wamekwenda kuzichezea timu zao za taifa.









0 COMMENTS:
Post a Comment