October 28, 2018


Kocha Mkuu wa timu ya JKT, Bakari Shime amesema baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Azam FC wamerekebisha makosa yao kuelekea kwenye mchezo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Uwanja wa Maj.Gen.Isamuhyo.

Shime amesema wamejipanga kiasi cha kutosha katika mchezo huu ili kuweza kutumia vizuri uwanja wa nyumbani.

"Makosa kwenye mchezo wetu uliopita tumeyafanyia kazi, tutapambana kuhakikisha tunapata pointi tatu muhimu kila mchezaji amejipanga na nimewaandaa kisaikolojia kuhakikisha tunaweza kupata matokeo," alisema.

JKT Tanzanzania wameanza vizuri msimu huu baada ya kufanikiwa kucheza michezo 10 wakiwa wamepoteza mchezo mmoja pekee na wameshinda michezo mitatu wametoa sare michezo sita wamejikusanyia pointi15 wakiwa nafasi ya 9.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic