Nahodha Msaidizi wa timu ya Yanga, Juma Abdul amewataka wachezaji kuendelea kujituma zaidi ili kuweza kupata matokeo katika mechi zinazokuja.
Abdul ambaye alikuwa anasumbuliwa na majeraha ameanza kurejea katika ubora wake baada ya kuanza kucheza akianzia benchi kutokana na mpango wa kocha kumtaka.
"Tumeweza kupata matokeo katika mchezo wetu wa jana , ila bado wachezaji tuna kazi ya kuendelea kupambana zaidi kupata matokeo kwa kuwa ushindani ni mkubwa, tunahitaji tuweze kushinda," alisema.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuwa nafasi ya pili baada ya kufikisha pointi 25 wakiwa na tofauti ya pointi 2 na vinara Azam ambao wana pointi 27.
Wachezaji wa Yanga wanaonekana kutumia zaidi nafasi wanapochezehwa na ajibu hivyo kocha anatakiwa kumtengeneza mchezaji mwingine kama alivyomtengeneza ajibu ili asaidie yaani awe mbdaa.w ajibu,hio liko wazi yang wanaeewa zaidi staili ya pasi za ajibu na kupta
ReplyDelete