KICHUYA AKANA KIWANGO CHAKE KUSHUKA, AFUNGUKA JUU YA KUTOITWA TAIFA STARS.
Na George Mganga
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba, Shiza Kichuya, amekanusha kushuka kwa kiwango chake tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara.
Kichuya ameeleza hilo kupitia swali aliloulizwa mdau wake kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuwataka mashabiki zake kumuulizwa maswali yoyote leo.
Mdau huyo alitaka kujua kwanini kiwango chake kimeshuka tofauti na msimu uliopita jambo ambalo limepelekea kutokucheka na nyavu hata mara moja msimu huu.
Lakini Kichuya alimjibu na kumueleza kuwa bado hajapata nafasi vema ya kutumia ila siku akipta anaamini atacheza vema na ikiwezekana atafunga pia.
Aidha, Kichuya alijibu moja ya swali lililomtaka kueleza amejisikiaje kutokuitwa Taifa Stars kwa kusema hayo ni maamuzi ya Kocha Mkuu huku akieleza anaweza akaitwa kwa wakati mwingine kwani bado anapambana.
0 COMMENTS:
Post a Comment