Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Stars, Emmanuel Ammunike ameweka wazi kwa kusema kuwa hawezi kumuita mchezaji yeyote ndani ya timu ambaye hajakamilika akiwemo Ibrahim Ajibu ila akiona anafaa anaweza kumuita.
Ajibu amekuwa akifanya vizuri ndani ya timu ya Yanga na kutoa mchango mkubwa Ligi Kuu Bara baada ya kuhusika kwenye mabao 11 kati ya 15 waliyofunga ila hajaitwa timu ya Taifa.
Ammunike amesema kuwa watu wanapaswa watambue kucheza timu ya taifa ni jambo lenye maana kubwa kwa mchezaji hivyo siyo kila mchezaji anaweza kuitwa kwa kuwa ni msaada kwenye klabu yake.
"Yapo mambo mengi ambayo yanazingatia mchezaji kuitwa timu ya taifa, mchezaji anatakiwa awe amekamilika na kujua nchi inataka nini na siyo kila mchezaji anayefanya vizuri anaitwa timu ya taifa, maana klabu na timu ya taifa ni vitu viwili tofauti, sisemi kwamba hatacheza ila nitakapoona anafaa naweza kumuita," alisema.
Stars inatarajiwa kuweka kambi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Lesotho kwa ajili a Kufuzu Fainali za Michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) Cameroon.
0 COMMENTS:
Post a Comment