KOCHA LIPULI: RATIBA INATUBANA
Kocha wa Lipuli FC ya mkoani Iringa, Seleman Matola baada ya kupoteza dhidi ya Singida United, kwa bao 1-0, ameibuka na kusema kuwa ratiba imewabana sana ndiyo maana wamepoteza.
Lipuli ambao Ijumaa wanajiandaa kucheza na Stand United katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa kwa sasa wanashika 11 wakiwa na pointi 11.
Matola alisema kuwa walijiandaa vizuri juu ya mchezo wao huo lakini ratiba inawabana sana pia ndiyo inachangia wao kufanya vibaya katika mechi zao kwani ndani ya wiki moja wamecheza mechi tatu.
“Ukiangalia ndani ya wiki moja tumecheza mechi tatu, tumecheza mechi Jumanne na KMC, tumecheza mechi Ijumaa na Azam na Jumatatu ndiyo hao Singida.
“Yaani hata wiki haujamaliza unacheza mechi, nafikiri tumepoteza mchezo huu kwa sababu ya uchovu tu,” alisema Matola nahodha wa zamani wa Simba na kiungo wa Super Sport ya Afrika Kusini.
0 COMMENTS:
Post a Comment