ZAHERA AHAMIA KWA DIAMOND PLATNUMZ, AMCHANA LIVE
Si kwenye soka pekee hata kwenye muziki yumo, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema kuwa huwa hapendi kusikiliza nyimbo za msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz sababu ni mjanjamjanja.
Kocha huyo ambaye ni raia wa DR Congo na Ufaransa ambako muziki ndiyo nyumbani kwake, amekuwa akifuatilia muziki wa hapa nyumbani lakini amevutiwa zaidi na AliKiba.
Kwa mujibu wa Championi Jumatano, kocha huyo alisema muziki wa hapa Bongo amekuwa akiufuatilia ingawa sio sana kama ulivyo wa kwao Congo.
“Muziki wa hapa ndiyo ninaufuatilia kwa kiasi fulani, najua kuna Diamond ila simpendi sana kwa sababu yeye ni mjanjamjanja kwenye mambo yake lakini napenda muziki unaoimbwa na AliKiba.
“AliKiba ni mwanamziki mzuri na muda mwingi nasikiliza muziki ule wa kwetu Congo na kufanya mambo yangu mengine ya soka,” alisema Zahera.
0 COMMENTS:
Post a Comment