October 3, 2018





Ule mkataba kati ya Yanga na kampuni ya vifaa vya michezo ya Macron, umeota mbawa.


Yanga waliingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni hiyo ambao ulielezwa utakuwa na thamani ya Sh bilioni tatu na ulisainiwa klabu hapo mbele ya waandishi wa habari.


Klabu ya Yanga, imethibitisha kuvunjika kwa mkataba huo ikieleza kwamba Macron ndiyo chanzo.

Msemaji wa Yanga, Dismas Ten amesema kwa kuwa Macron walishinda kutekeleza makubaliano karibu yote waliyoingia kupitia mkataba huo, basi umevunjika.

"Maana hata jezi utaona klabu kwa sasa inajinunulia., maana yake hakuna mkataba tena na Macron," alisema Tena.

3 COMMENTS:

  1. WAPENI MAJIBU WANACHAMA NA WAPENZI WENU LINI MATENGENEZO YA UWANJA WA KAUNDA UTAISHA? WAPENI MAJIBU YA UANZAJI WA MIPANGO YA JEZI, UCHAGUZI, A LINI MANENO YANAKUWA VITENDO????MMEHAIDI SANA!!!!! SASA NI WAKATI WA VITENDO......KWENYE YAFUATAYO
    1. UWANJA WA KAUNDA
    2. KOCHA MSAIDIZI WA KUMSAIDIA ZAHERA.....WATU WAMEONA MAPUNGUFU NI DHAHIRI KUWA BENCHI LA UFUNDI LINAHITAJI KUIMARISHWA KAMA MNATAKA KUCHUKUA UBINGWA
    3. UCHAGUZI
    4. MABADILIKO YA MFUMO WA UENDESHWAJI
    5. USAJILI WA DIRISHA DOGO MMESHAANZA KUWATAFUTA WACHEZAJI WA KUONGEZWA NA KUWAPA MIKATABA YA AWALI?

    ReplyDelete
  2. Mkataba umevunjika vipi?Viongozi bongo lala mlisaini mkataba bila ya kifungu cha kulipa fidia kwa aliyesababisha mkataba uvunjike au kushindwa kutimiza masharti ya mkataba. Ni wakati muafaka tuchague viongozi wapya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na mimi nashangaa. Mkataba wa Bilioni tatu hauna kipengele cha kuwajibika kwa mvunjaji..? Kweli Tanzania kuna vituko.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic