Yanga itamkosa kocha wake Mwinyi Zahera wakati ikishuka uwanjani kuwavaa Mbao FC wikiendi hii.
Msemaji wa Yanga, Dismas Ten amesema Zahera hatakuwepo nchini kwa kuwa ataungana na timu ya taifa lake ya DR Congo itakayokuwa ikipambana kuwania kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika.
"Kwa hiyo kocha hatutakuwa naye, lakini kila kitu kipo katika mpangilio na vijana wako tayari kwa kuwa wamekuwa na kocha muda wote," alisema.
Zahera bado ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DR Congo na mmoja wa makocha wazalendo wa nchi hiyo wanaoaminika.
WAPENI MAJIBU WANACHAMA NA WAPENZI WENU LINI MATENGENEZO YA UWANJA WA KAUNDA UTAISHA? WAPENI MAJIBU YA UANZAJI WA MIPANGO YA JEZI, UCHAGUZI, A LINI MANENO YANAKUWA VITENDO????MMEHAIDI SANA!!!!! SASA NI WAKATI WA VITENDO......KWENYE YAFUATAYO
ReplyDelete1. UWANJA WA KAUNDA
2. KOCHA MSAIDIZI WA KUMSAIDIA ZAHERA.....WATU WAMEONA MAPUNGUFU NI DHAHIRI KUWA BENCHI LA UFUNDI LINAHITAJI KUIMARISHWA KAMA MNATAKA KUCHUKUA UBINGWA
3. UCHAGUZI
4. MABADILIKO YA MFUMO WA UENDESHWAJI
5. USAJILI WA DIRISHA DOGO MMESHAANZA KUWATAFUTA WACHEZAJI WA KUONGEZWA NA KUWAPA MIKATABA YA AWALI?