October 16, 2018





Mwanasheria wa Zacharia Hans Poppe amesema mteja wake hakukamatwa kwa kuwa aliwasiliana na Takukuru kabla ya kurejea kutoka Marekani.

Augustine Dominic Shio pamoja na Benect  Alex wamesema Hans Poppe hakukamatwa kama ilivyoelezwa badala yake alikwenda mwenyewe hadi Takukuru.

"Alikwenda Takukuru na kuhojiwa na baada ya hapo walimuachia akaenda kwake kupumzika, halafu leo akafikishwa mahakamani.

"Kabla ya kuja pia aliwasiliana na Takukuru kuhusiana na kurejea kabla ya kutoka Marekani," alisema.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe ameachiwa kwa dhamana baada ya kusomewa mashitaka mawili katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Shitaka la kwanza :Kutoa taarifa ya uongo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusiana na nyasi bandia, kwamba alitaja bei kubwa zaidi.

Shitaka la pili:Nyaraka za nyasi bandia hazikuwa za ukweli, anatuhumiwa kuzigushi.

Dhamana yake ina thamani ya Sh. milioni 30 kwa watu wawili, kila mmoja akiweka  Sh milioni 15.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Ijumaa Oktoba 19 itasikilizwa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic