October 12, 2018


Kila mtu leo anaiombea timu yetu ya taifa, Taifa Stars ili iweze kupata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Cape Verde.

Hakika ni mchezo ambao kila mmoja anausubiri kwa hamu kubwa sana na ushindi tu ndiyo unaweza kutusaidia sisi kusonga kuwa na matumaini kwenye mchezo huo.

Wengi wanaamini kuwa kwa sasa timu yetu ipo vizuri na inaweza kupata ushindi kwenye mchezo wowote ulioko mbele yao.

Hakika ni jambo la kusubiri na tuzidi kuwaombea lakini ukifuata rekodi vizuri utagundua kuwa mara nyingi tumeshindwa kupata matokeo mazuri kila tunapokutana na taifa hili.

Sawa ni kweli, lakini haimaanishi kuwa rekodi inacheza uwanjani, wakati tunacheza na Cape Verde huku nyuma hatukuwa na mchezaji hata mmoja wa kimataifa, tulikuwa tukitegemea Simba na Yanga tu ndiyo zitupe wachezaji, lakini leo tunakwenda tukiwa timu nyingine kabisa.

Tunkwenda tukiwa na wachezaji zaidi ya saba ambao wapo kwenye kikosi chetu na hivyo wenyeji wetu nao sasa wanagundua kuwa wanakutana na timu bora zaidi kwa sasa kwenye soka la Afrika.

Ushindi kwa Stars kwenye mchezo huu utawafanya kuwa kwenye kasi nzuri zaidi kwa kuwa watafikisha pointi tano kama Uganda atafungwa na Lesotho ina maana kuwa Taifa Stars watakuwa kileleni kwenye kundi.

Lakini jambo la kufurahisha ni kwamba siku nne baadaye Stars itakuwa hapa nyumbani kuvaana tena na timu hiyo na kama itashinda michezo yote miwili ina maana kuwa itafikisha pointi nane na hivyo kama itapata pointi kwenye mchezo wake mwingine dhidi ya Lesotho basi itakuwa nafasi kubwa kwa timu hiyo kufuzu.

Ni vizuri tukiwaombea kuhakikisha kuwa wanapata ushindi kule, lakini wakati mwingine naona kuna tatizo kubwa kwenye uchaguzi wa wachezaji wa timu hii.

Nafikiri kuna wakati tunatakiwa kuwa wakweli hata kama kazi ya kuchagua ni ya kocha, lakini kuna vitu vinaonekana kutokuwa vizuri na hata kama Stars watapoteza mchezo wa leo lazima lawama zitakuwepo.

Ni jambo la ajabu Stars kuwa bila mshambuliaji bora kwa sasa hapa nchini, Eliud Ambokile, jiulize mshambuliaji ndiye mchezaji bora kwenye ligi kwa sasa, ndiye kinara wa mabao, amefunga mabao sita halafu hayupo kwenye kikosi cha Taifa Stars.

Nafikiri kuna tatizo hata kama kocha alikuwa hamtaki, lakini kumwita kungempa morali ya juu zaidi na kuendelea kupambana, lakini kama hamtumii leo basi angeanza kumuandaa kwa ajili ya miaka kadhaa mbele.

Nafikiri wakurugenzi wa benchi la ufundi la Stars wanatakiwa kumshauri wakati mwingine kwa maendeleo ya soka la nchi hii.

Pia mchezaji anayeonyesha kiwango cha juu zaidi kwa sasa kwenye ligi ni Ibrahim Ajibu ambaye hadi sasa ndiye mchezaji aliyehusika kwenye mabao mengi zaidi kwenye ligi kuliko mwingine yoyote.

Sijui kwa nini kocha hakumwita Ajibu, lakini ni jambo la ajabu kumuacha kiungo mshambuliaji kama huyu kwenye timu yetu ya taifa.

Nafikiri kocha anaweza kusema kuwa atamwita siku nyingine, lakini kwangu naamini haitakuwa sawa kwa kuwa hakuna anayefahamu kama Ajibu atabaki kwenye kiwango alichonacho sasa kwa muda gani.

7 COMMENTS:

  1. Uwezo wa mchezaji na nafasi ya kucheza ni mambo mawil tofaut. Una uwezo lakn mfumo wangu haukuhitaj. Unaonaje nakuita alaf unakaa bench?hapa utagundua tunachagua kutokana na mfumo ninaokwenda kutumia. Embu twende tukapambane kwanza tuache haya na yale

    ReplyDelete
  2. Wachambuzi wa bongo sijui wanakulaga mavi wanamwona ajibu tuu kwa kuwa ndoo anaweza kuwapa matokeo kisa kafunga juzi ukiona ivyoo ni sababu wachambuzi wanatafuta tukifungwa utasikia kwann walimwacha ajibu bwege kweli

    ReplyDelete
  3. Uchambuzi wa kitoto ambao sijawahi kuuona....nani alikuambia stars inatatizo la striker....? Mm nafikir tumalize game afu tujadiliane

    ReplyDelete
  4. Mbona kuna wachezaji wazuri zaidi ya Ajibu wameachwa! Hivyo kweli

    ReplyDelete
  5. Upo sawa mchambuzi kwasababu jina la ajibu ni pressure kwa wapinzani

    ReplyDelete
  6. Kaka salehe jembe,nilikiwa nafiatilia sana blog yako na habari zako lakini kwa hili siungi mkono,tuacheni usimba na uyanga mchezaji kweli unampima kwa mechi zipi? Huwezi kumpima ajibu kwa mechi za stand,ndanda,n.k anhalia Ajibu akicheza na Azam,au Simba mini anafanya hamalizi game anashindwa kuthibitisha ubora huo,hata ambokile pia bado hajafikia ubora huo,so kama no wabaya lakini uwezo bado kwa kweli ,hats hao walioitwa stars kulinganisha na wenzetu nasema baado,Mimi no mzalendo na sipendi uyanga na usimba uingie kwenye taifa stars lakini ajibu apambane sana kwani ajibu ana kitu kikubwa sana miguuni make Ila bado hajakitambua akipambana naamini ana uwezo was kucheza hats ulaya lkn kwa alivyo sasa bado.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kaka Salim haya sasa unaweza kuongea yale uliyokuwa ukimshambulia mchambuzi wa Makala hii hapo jana.Saleh ni mchambuzi aliyebobea kwenye anga za michezo hivyo alichokuwa anakiongea alimaanisha,acheni unazi wa Simba na Yanga hadi kukosoa pasopostaili.
      Saleh endelea kutupa habari na tuelimishe kuhusu michezo acha hao wasiojua soka walalame

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic