October 22, 2018


Uongozi wa timu ya Azam FC, umesema kuwa wachezaji wao wawili Frank Domayo na Paul Peter wataukosa mchezo unaofuata dhidi ya timu ya JKT Tanzania kutokana na kuendelea kusumbuliwa na majeraha.

Ofisa habari wa Azam FC, Jaffari Maganga amesema kuwa mchezaji Paul Peter atakuwa nje kwa muda wa miezi miwili baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Afrika kusini.

"Tumejipanga vizuri kuhakikisha kwamba tunafanikiwa kuendelea kupata ushindi hasa kwa michezo yetu inayofuata na tunajua kwamba tunawafuata JKT nyumbani mchezo ambao utakuwa mgumu  tupo tayari.

"Wachezaji wote wapo vizuri ili kuweza kupata point tatu na hilo lipo kwenye uwezo wetu tayari tumeshaanza mazoezi kujiandaa na mchezo wetu unaofuata"alisema .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic