Bondia Hassan Mwakinyo amesaini mkataba wa miaka mitatu na kampuni kubwa zaidi ya kubashiri nchini ya SportPesa.
SportPesa imesaini mkataba huo na kuutangaza leo ingawa ni kiasi gani imefanywa kuwa siri.
Mkataba huo kati ya Mwakinyo na SportPesa umesainiwa mbele ya waandishi wa habari na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.
Baada ya kusaini mkataba huo, Dk Mwakyembe aliwapongeza SportPesa kuamua kuingia kwenye ngumi na kumuamini Mwamkinyo.
“Hili ni jambo zuri sana, kwa kweli SportPesa wanastahili pongezi katika suala hili,” alisema.
“Kikubwa sasa ni kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha tunawavutia wengine zaidi.”
Naye Mkurugenzi wa SportPesa, Abbas Tarimba alisema wameendelea kujitanua katika baada ya kufanya vizuri katika michezo kupitia soka.
“SportPesa tuko sehemu nyingi duniani, wenzetu kama Kenya wamejitanua hadi kwenye rugby, kwingine pia kuna michezo mingine. Hapa tulianza na soka na baada ya mafanikio, sasa tunaingia kwenye ngumi na tumeanza na Mwakinyo lakini tusisitize, mkataba wetu utabaki kuwa siri,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment