Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni Dk Harrison Mwakyembe amewataka wadau wa mpira kuisaida timu ya Taifa Stars ili kuweza kuweka kambi nchini Afrika Kusini kujiandaa na mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).
Stars itacheza na Lesotho mwezi ujao ukiwa ni mchezo wa marudio baada ya kutoka sare mchezo wa kwanza uliochezwa nyumbani huku mashindano hayo yakitarajiwa kufanyika mwakani nchini Cameroon.
“Tunawaomba mchango kuelekea mchezo wa Lesotho, kwa ajili ya gharama za kusafirisha timu yetu ya Taifa, bajeti imeongezeka kwa kuwa tutaweka kambi Afrika Kusini.
“Tunafanya mazungumzo kwa kushirikiana na TFF na mashirika ya Ndege, makampuni ya magari ili kupata bei nzuri kwa watanzania wengi waweze kusafiri," alisema.
Stars ipo kundi L imecheza michezo minne na kupoteza mchezo mmoja na wamepata sare mbili na wameshinda mchezo mmoja na kuwafanya wakusanye point 5 na kushika nafasi ya pili.
Wazo zuri na lifanyiwe kazi kikamilifu. Kushinda mechi ni maadalizi ya kimkakati ya bila ya kuchoka kuanzia siku ya tarehe tajwa ya siku ya mechi kama vile kupeleka watu wa kufuatilia hata sasa japo wakwenda na kurudi au hata kuwaskauti watanzania wanaoaminika wanaoishi kule kufuatilia maandalizi ya mpinzani wetu yakoje na mambo mengine ya muhimu. Mara hii lazima kieleweke na hata ikitokea bahati mbaya hatukupita basi kila mtanzania lazima ajiulize alifanya nini kuisadia timu kuhakikisha inapata matokeo tunayoyataka?
ReplyDeleteYea
ReplyDeleteMungu atakuwa upande wetu, wadau tuiunge mkono timu yetu kwani kila kitu kizuri kinahitaki maandalizi mazuri
ReplyDelete