Ofisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPL), Boniphace Wambura amesema wameamua kusogeza mbele baadhi ya mechi kupisha maandalizi ya timu ya taifa itakayoweka kambi Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) dhdi ya Lesotho.
Mechi hizo pamoja na ile ya African Lyon na Yanga iliyopangwa kufanyika Novemba 7, Simba na KMC FC, Azam na Mbao FC yote itachezwa Novemba 8, pia wamepanga tarehe ya viporo vya mechi za Simba,Yanga na Azam.
"Mechi ya Yanga na Mwadui itakuwa Novemba 21, Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Simba na Lipuli FC, Uwanja wa Taifa Novemba, huku ule wa Azam na Ruvu Shooting utachezwa Novemba 22, Uwanja wa Chamazi.
"Tumeamua kupeleka mbele ratiba za mechi ligi kuu ili kuweza kutoa nafasi kwa ajili ya maandalizi ya timu ya Taifa kupata muda wa kutosha kujiaanda, malengo yetu kuona ikikata tiketi ya kushiriki Afcon mwakani nchini Cameroon," alisema.
Stars inatarajiwa kwenda Lesotho Novemba 18, inashika nafasi ya pili kwenye kundi L baada ya kucheza michezo minne na kushinda mchezo mmoja, imetoa sare michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja na kujikusanyia pointi 5.
0 COMMENTS:
Post a Comment