October 12, 2018


Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limemshangaa kocha wa Simba, raia wa Ubelgji Patrick Aussems aliyedai kwamba wachezaji wake wanapewa mazoezi makali ndani ya Taifa Stars ndio maana wanapata majeraha.

Aussems aliwashushia lawama hizo TFF baada ya mchezo wa Simba na Africa Lyon kwa akiwataja zaidi Shomari Kapombe na Jonas Mkude.

Lakini Ofisa habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema kuwa ni jambo la ajabu hasa kwa mwalimu kusema kuwa mazoezi yanawaumiza wachezaji kwani wanajengwa kwa mazoezi.

“Uwezo wa mchezaji unaongezeka kutokana na mazoezi na kama wao wanalalamika suala hilo basi kuna tatizo hasa kwa wachezaji wenyewe kuwa wavivu kufanya mazoezi ama mazoezi wanayopewa ni rahisi hivyo wamekutana na ugumu ambao umewashtua.

“Timu ipo kwenye maandalizi ya kucheza na Cape Verde hivyo uimara unahitajika ili wachezaji waweze kupambana kiasi kikubwa na kama watafanya mazoezi kidogo jambo hilo halileti afya kwenye soka la ushindani,” alisema Ndimbo.

5 COMMENTS:

  1. Kocha wa simba amehoji kitaalamu aliyetakiwa kumjibu ni mtu mwenye utaalamu kama wake huyo ndimbo asikurupuke kujibu mambo ambayo yako nje ya fani yake

    ReplyDelete
  2. Waandishi vilaza ...
    Mazoezi hayafanywii kama kuku Lazma kuwe na program maarum...

    ReplyDelete
  3. Mazoezi, magumu halafu unatakiwa ucheze mechi ngumu ukiwa bado kwenye mazoezi, si sawa. Ligi ingeahirishwa kisha kambi ya stars iendeleeeeee.

    ReplyDelete
  4. Mazoezi, magumu halafu unatakiwa ucheze mechi ngumu ukiwa bado kwenye mazoezi, si sawa. Ligi ingeahirishwa kisha kambi ya stars iendeleeeeee.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic