UTETEZI WA ALIKIBA BAADA YA KUFUTA VIDEO YAKE 'HELA' YOUTUBE
Staa wa Bongo Fleva, Alikiba, ambaye siku ya jana alikumbana na lawama na kejeli za mashabiki wake mitandaoni baada ya kufuta wimbo wake mpya wa ‘HELA’ aliouachia usiku kupitia mtandao wa YouTube kisha kuufuta asubuhi, amefunguka sababu za kufuta wimbo huo.
Alikiba ametaja sababu kubwa ya kufuta wimbo huo ni siku ambayo aliachia, kwani haikuwa siku ambayo huitumia kuachia nyimbo mpya.
“Siku yenyewe haikuwa siku yangu ambayo napenda ku-release nyimbo, ilikuwa siku ya Jumanne, so tukamwambia jamaa autoe, inatakiwa siku kama ya leo Alhamisi, ndiyo maana ulikuta umetoka kwenye YouTube, ila sasa hivi ukiingia utaikuta”, amesema Alikiba.
Alikiba amelazimika kutoa maelezo hayo baada ya kushambuliwa na mashabiki kuwa ameutoa wimbo huo kwa kuwa ni mbaya huku wengine wakidai amerudia wimbo wake wa zamani.
0 COMMENTS:
Post a Comment