Kikosi cha Taifa Stars, kimeendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
Taifa Stars chini ya Kocha Emmanuel Amunike imeendelea na mazoezi kwenye uwanja huo huku kocha huyo Mnigeria akiendelea kutoa mbinu kadhaa.
Kikosi hicho kinajifua kuwania kuwavaa Cape Verde katika mechi za kuwania kufuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika.
Stars na Cape Verde, zitacheza mechi mbili ndani ya siku nne pamoja na kusafiri safari ndefu za takribani saa 18 ndani ya siku tano.
0 COMMENTS:
Post a Comment