October 4, 2018


Mshambuliaji wa timu ya Mbeya City ya mkoani Mbeya, Eliud Ambokile amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Septemba wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019. 

Ambokile alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Ibrahim Ajibu wa Yanga na Stamili Mbonde wa Mtibwa Sugar alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam wiki hii na Kamati ya Tuzo ya TPL.

Tuzo hiyo mara ya kwanza kwa msimu huu ilichukuliwa na straika wa Simba, Meddie Kagere baada ya kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi katika mechi mbili za mwanzo dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City.


1 COMMENTS:

  1. Magumashi ya soka la Bongo Ambokile kachaguliwa mchezaji wa mwezi na hayupo kwenye wachezaji 30 wa timu ya Taifa.Nani kamchagua na nani kamwacha?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic