November 22, 2018


Beki wa timu ya Taifa ya Tanzania, Abdi Banda anayechezea timu ya Baroka FC ya Afrika Kusini, amesema kupoteza mchezo wao dhidi ya Lesotho umemfaya apoteze furaha, ila bado ana imani ya kuweza kupata matokeo kwenye mchezo wao dhidi ya Uganda.

Katika mchezo huo uliochezwa nchini Lesotho, Banda hakucheza na taarifa zikasambaa kuwa ameshindwa kuelewana na Kocha Mkuu, Emmanuel Amunike na kuhusika kupanga kikosi kilichopoteza.


"Watanzania inabidi watambue kuwa maneno yanayosambazwa juu yangu hayana ukweli, ni thamani kubwa sana kucheza kwenye timu ya Taifa, sina uwezo wa kumpangia kikosi mwalimu sijafikia hatua hiyo maana benchi la ufundi ni pana.


"Mwalimu alikuwa na mipango yake hivyo ulikuwa ni wakati wa wengine kupewa nafasi, kufeli kwa mbinu yake kunafanya mashabiki watafute sababu jambo ambalo halina ukweli, nguvu yetu tumewekeza  kwenye mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Uganda," alisema.

4 COMMENTS:

  1. Heko Abdi Banda,Umeuelewa mfumo Wa Moira.Ujue Moira Wa Tz unapangwa na magazeti,unapangwa na mashabiki.magazeti yanakuwa na oroza ya wachezaji mkononi kumpa kocha,wasipo waona basis huleta shida.Amulike ni boƱge LA kocha tumtumie vizuri.Wenye bifu na Amulike waache kuchafya Moira Wa Tz.kwani ni mpaka acheze mkude ndipo ihesabike time ni nzuri?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mfyuu bonge la Kocha kwako wewe Jorom.Kuchezea Barcelona ndio uweweseke kuwa ni bonge la Kocha? Dondosha basi CV yake utuaminishe kuwa ni bonge la kocha.

      Delete
    2. Huyu JOROM atakuwa sio Mtanzania huyu kama mwenzake Amunike.

      Delete
  2. Amunike bonge la kocha?! Unashangaza sana. Tuambie alifundisha timu gani na kuipa mafanikio? Hakuna kocha hapo, ni ufyoro mtupu! Kocha hajui kuchagua wachezaji, hajui kupanga kikosi na hawezi hata kuusoma mchezo! Kocha gani huyo?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic