November 30, 2018

Uongozi wa Azam FC, umesema kuwa wameongeza nguvu kubwa Ligi Kuu kutokana na ushindani uliopo ili waendelee kuweza kulinda rekodi ambayo wameanza nayo msimu huu.

Meneja wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa mipango imekaa sawa na nguvu kubwa kwa sasa ni kwenye mchezo wao wa ligi kuu unaofuata dhidi ya Stand United.

"Ushindani ni mkubwa jambo ambalo linazidi kutupa nguvu na kutufanya tufikirie kupata matokeo mazuri zaidi, kwa sasa timu ipo kwenye maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Stand United, tunawaheshimu wapinzani wetu hivyo tumejipanga kufanya vizuri," alisema.

Azam FC wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wamecheza michezo 13 bila kupoteza wameshinda michezo 10 na kutoa sare 3 wana pointi 33 tofauti ya pointi 2 na Yanga ambao ni vinara wa Ligi kwa sasa wakifuatiwa na Simba.

1 COMMENTS:

  1. Zenu nyie ni mbwembwe tu mwisho wa siku bingwa ni yanga au simba tumeshawazoea azam jaribuni kwenye like kombe lenu labda mtafanikiwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic