November 30, 2018


Kutokana na mshambuliaji wa Azam FC ambaye amesajiliwa akitokea timu ya Nogoom FC ya Misri, Obrey Chirwa kusema kama hatalipwa stahiki zake kwa wakati atavunja mkataba, uongozi umemtuliza.

Hivi karibuni Chirwa ambaye alikuwa kinara wa migomo kwenye kikosi cha Yanga alihojiwa na kusema kama hatalipwa fedha zake na timu hiyo atavunja mkataba.

Kwa mujibu wa Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Iddi, amesema kuwa kikubwa ambacho wanakisimamia ni haki na usawa hasa kwa wachezaji wote ndani ya timu hiyo.

“Hakuna wasiwasi ndani ya Azam FC, kwa kuwa uhakika wa kukamilisha malipo kwa wakati upo hivyo kikubwa Chirwa anatakiwa afanye kazi na asifikirie kuhusu kutolipwa ndani ya timu yetu.

“Tuna kazi kubwa ya kuweza kuendelea kuwa bora zaidi ya jana hivyo ili tuimarike ni lazima tufanye kweli hasa kutokana na ushindani ambao upo kwenye ligi tutapambana ili kuendelea kutunza rekodi ya kutofungwa,” alisema Iddi

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic