November 29, 2018




Baada ya mashabiki wa Simba kulalama inakuaje uongozi wa Azam FC kuwasaidia wapinzani wao Mbabane Swallows FC kwa kuwapatia basi lao kwa ajili ya kuwapeleka mazoezini pamoja na uwanjani wakati wao ni wapinzani wao wa kubwa, uongozi wa timu hiyo umeibuka na kutema cheche na kusema kuwa wao na uongozi wa Simba walikubaliana kabla.


Jana Simba walicheza na Mbabane katika mechi ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa ya Afrika ambapo walikuwa wanaonekana na basi la Azam katika sehemu mbalimbali kabla ya kuivaa Simba.


Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu yao, Mzizima Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd alisema kuwa wamepokea malalamiko kwa mashabiki wa Simba kupitia chombo cha habari cha Salehjembe ambapo kiliandika taarifa jana ambapo wanaishutumu klabu yao kwamba inawahujumu wakiona ni ya Tanzania lakini inawasaidia wageni.


“Tumepokea malalamiko kwa mashabiki wa Simba kupitia chombo cha habari cha Salehjembe ambapo kiliandika jana taarifa kwa mashabiki wakishutumu Azam ambapo naomba ni nukuu chombo hicho kilisema mashabiki wa timu ya Simba wanashangazwa na uongozi wa Azam FC kuruhusu wapinzani wao kutumia basi lao Mbabane Swallows FC, Mbabane walitumia basi la Azam walipoenda kufanya mazoezi Uwanja wa Taifa.

"Basi tulilitoa baada ya Simba kutuomba, walisema wanahitaji basi kwa ajili ya matumizi ya Mbabane Swallows. Walisema wataweka wataweka mafuta wenyewe kwa muda timu hiyo itakapoondoka. Hapa utaona kuwa Simba yaani uongozi wanajua kuwa tuna ushirikiano na kwa nini Mbabane wametumia basi letu.


“Naomba jambo hili niliweke vizuri suala ambapo chombo hichi cha SALEHJEMBE kiliandika kuwa mashabiki wana hofu ya Azam inahusika kuijumu Simba na kuipatia basi wapinzani wao kwa kutumia kwa kipindi chote watakapo kuwepo hapa wakijiandaa na mechi yao na baada ya kucheza jana kutumia basi la Azam  ni watu kutoelewa tu.


"Tunakodisha malori yanayobeba unga, tunakodisha vitu mbalimbali. Lakini kuhusiana na suala la mabasi, mara nyingi kwa wadau wakiwemo TFF au klabu huwa tunasaidiana tu, wao wanaweka mafuta na kuwapa posho madereva.


“Kwa hiyo sisi hatukuwapa hao Mbabane kama mashabiki walivyoamini wakilalamika kupitia Blog ya Salehjembe inavyosema na wala hatuhusiki kwa njia moja ama nyingine kwa sababu Simba SC iliandika barua kuomba basi letu kwa ajili ya wageni wao ambao ni Mbabane nadhani Simba nao wanatakiwa kutoa statiment kwa mashabiki wao kwamba hakuna ujuma ya Azam kutumika au kwa njia yoyote kuwa Azam ilitumika kuihujumu Simba, wale ni wageni wao na sisi tumeshiriki kama sehemu hiyo ya kusaidiana na Simba ambao wana majukumu ya kimataifa."

"Lakini pia ndugu zetu African Lyon nao walikuja hapa kukodi basi na timu kubwa kutoka Marekani ilikuja na walitumia na kanuni za Caf wameondoa utaratibu timu mgeni kupewa hoteli kwa sababu mara nyingi timu zinakuwa zinapewa au zinafikia katika hoteli ambazo sio nzuri kwa hiyo wakakiondoa kipengele hicho cha hoteli na utaratibu waliotuachia ni kwamba mwenyeji atampa mgeni usafiri mgeni wake anapokuja katika mashindano ya Caf na ndiyo Simba walichofanya hivyo kwa kukodi sisi kwetu na kuwapa wageni wao,” alisema Jaffar maarufu kama Mbunifu.


MHARIRI;

Tuweke msisitizo kwamba stori iliyoandikwa ilikuwa na maoni ya mashabiki na wanachama wa Simba. Lakini kama waungwana, tuwaeleza Azam FC hivi;

Kama kutakuwa na usumbufu uliojitokeza kwa Azam FC ambao ni wadau wetu katika suala la habari, TUNAWAOMBA RADHI SANA.
     

2 COMMENTS:

  1. Mnajua kuwa kunatakiwa kubalance story kabla ya kupublish lakini kwa kiherehere mkaandika moja kwa moja kabla ya kuwasiliana na Azam. Jifunzeni kufata media ethics...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic