November 4, 2018


Na George Mganga

Crescentius Magori amechaguliwa kuwa Mtendaji Mkuu (C.E.O) atakayeiongoza klabu ya Simba baada ya kuchaguliwa na Bodi ya Wakurugenzi.

Magori ametangazwa leo katika Mkutano Mkuu wa Wanachama unaofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu J.K Nyerere jijini Dar es Salaam.

Uteuzi huo utaenda sambamba na uchaguzi ambao utafanyika hapo baadaye kwa ajili ya kuwapata viongozi wengine watakaoingoza Simba kwa miaka minne ijayo.

Simba inafanya uchaguzi huo kwa mara ya kwanza ikiwa katika hatua za mwisho kuelekea kukamilisha kwa mchakato wa mabadiliko kutoka mfumo wa zamani wa wanachama kwenda kiuwekezwaji.

Mpaka sasa wanachama wa klabu hiyo wanazidi kumimikika mkutanoni hapo kwa ajili ya kupiga kura hapo baadaye kumpata Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic