November 4, 2018


Kocha mkuu wa timu ya Kagera Sugar Meky Mexime amesema kuwa watatibua rekodi ya timu ya Azam FC ya kutopoteza mchezo hata mmoja mpaka sasa kwa kuwa rekodi zinawabeba hasa wanapokutana na vigogo wakubwa.

Kagera Sugar walifanikiwa kuitibulia Simba msimu uliopita kwenye mchezo wao wa mwisho baada ya kuwapiga bao 1-0 mbele ya Rais John Magufuli  ambaye alisema kuwa Simba walicheza vibaya hali iliyofanya wakaruhusu kutobolewa tundu.

 Maxime amesema kuwa wamejiandaa kiasi cha kutosha kuweza kupata ushindi mbele ya mabingwa wa Afrika Mashariki na kati watahakikisha wanafanikiwa kushinda nyumbani kwakuwa mchezo uliopita walipoteza dhidi ya Mtibwa Sugar.

"Hakuna mwalimu ambaye anafikiria kupoteza pointi tatu licha ya matokeo muda mwingine kuwa tofauti na vile ambavyo umefikiria ila hilo halitupi shaka kwa kuwa tuna kikosi makini cha ushindani.

"Nina maumivu ya kupoteza mchezo wangu wa kwanza dhidi ya Mtibwa hivyo nami pia ninapaswa nitibue rekodi ambayo inashikiliwa na Azam FC kwa sasa hilo litawezekana kwa wachezaji kucheza kwa juhudi na mashabiki kujitokeza kwa wingi kutoa sapoti," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic