November 27, 2018

Baada ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa Novemba 15 tayari timu kadhaa zimeingia sokoni na kukamilisha usajili kwa wachezaji pamoja na walimu kama ilivyo kwa Alliance FC huku nyingine zikiendelea kukamilisha mazungumzo.

Azam FC walianza kumtambulisha mshambuliaji Obrey Chirwa na kumpa kandarasi ya mwaka mmoja akiwa ni mchezaji huru kutoka timu ya Nogoom ya Misri.

KMC walifuata kwa kumpa kandarasi ya mwaka mmoja Elias Maguli wakamtambulisha mchezaji kutoka Singida United Salum Chuku ambaye ni beki wa kushoto kwa kandarasi ya mwaka mmoja.


Wachezaji wengine ambao wameshasajiliwa kwenye dirisha dogo ni pamoja na Miraji Adam kutoka Singida United amesajiliwa Coastal Union, Dauda Bortu amesajiliwa na Singida United kutoka Liberia.


Alliance FC ya Mwanza wamempa kandarasi ya miaka miwili kocha Malale Hamsini kutoka Ndanda FC kuziba nafasi ya Mbwana Makata aliyejiuzulu kwa madai ya kuingiliwa mamlaka na Mkurugenzi wa kituo hicho James Bwire.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic