November 27, 2018


Timu ya Azam FC, imewatoa wachezaji wake wanne kwa mkopo kwenye dirisha dogo ili waweze kupata nafasi ya kucheza katika timu nyingine.

Meneja wa Azam FC, Philip Alando amesema wamefikia hatua hiyo baada ya kuafikiana na timu pamoja na wachezaji kuzitumikia timu hizo.


Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23, Mbaraka Yusuf ataitumikia timu ya Namungo FC ya Mkoani Mtwara inayoshiriki Ligi daraja La Kwanza.

"Tumewatoa wachezaji kwa mkopo ambao ni pamoja na Ditram Nchimbi ataitumikia Mwadui, Waziri Junior ametolewa kwenda Biashara United, Abdul Haji ametolewa kwenda Mbao FC na Mbaraka Yusuf atakuwa Namungo ya Ligi daraja la kwanza," alisema Alando.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic