November 29, 2018


Mambo ni moto! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya mshambuliaji wa Yanga raia wa DR Congo, Heritier Makambo kuandika rekodi ya pekee hivi karibuni katika michuano ya Ligi Kuu Bara.

Makambo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kwenye Ligi Kuu Bara kufunga mabao kwenye michezo miwili mfululizo ya mkoani na kuwazidi Emmanuel Okwi pamoja na Mnyarwanda, Meddie Kagere wa Simba.

Makambo alifunga kwenye mechi dhidi ya Mwadui FC pamoja na Kagera Sugar ambazo zote Yanga walishinda.

Ilianza dhidi ya Mwadui FC, Novemba 22, mwaka huu katika Uwanja wa Kambarage Shinyanga na katika mchezo huo Makambo aliifungia timu yake hiyo bao moja kati ya mabao ya mawili iliyoshinda.

Baada ya hapo Yanga ilipambana na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba na katika mechi hiyo Makambo alifanikiwa kuifungia timu hiyo kwa mara nyingine bao moja kati ya mabao mawili ambayo iliyapata kwenye mchezo huo.

Hali hiyo imemfanya Makambo ambaye sasa ameshazifumania nyavu mara sita tangu kuanza kwa ligi kuu msimu huu kuandika rekodi ya pekee na kuwazidi Okwi na Kagere ambao kila mmoja katika mechi mbili za mikoani walizocheza mfululizo dhidi ya Mbao pamoja na Mwadui FC, Kagere tu ndiye alifunga bao moja.

Katika hatua nyingine, pia unaweza kusema kuwa Makambo ameonyesha kuwa ni moto wa kuotea mbali kwenye viwanja vya mikoani tofauti na Okwi pamoja na Kagere.

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic