November 29, 2018


Baada ya Simba kuwalaza vema Mbabane Swallows ya Swaziland jana kwenye Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harisson Mwakyembe, ametoa pongezi wa wekundu hao wa Msimbazi.

Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mbabane na kuifanya iwe na faida nzuri ya mabao mengi ambapo katika mechi ya marudiano watahitaji kwenda sare tu ili kuendelea mbele.

Mwakyembe amesema ni jambo jema kwa serikali kuona Simba inafanya vizuri kwani inapeperusha vema bendera ya Tanzania na inautangaza vema mpira wetu.

Aisha, Mwakyembe amewaasa Simba wasije wakabweteka kwa ushindi huo ili wasije kufungwa ugenini Disemba 4 ambapo Mbabane watakuwa kwao Swaziland.

"Ni jambo jema, tunawapongeza kwa kuwa wameanza vizuri, ni vizuri wakaacha kubweteka sasa kwasababu wana mchezo wa marudiano huko ugenini wiki ijayo" alisema.

Ukiachana na Simba, Mwakyembe pia amewapongeza Mtibwa Sugar ambao waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Northern Dynamo hapo juzi kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic