November 4, 2018


Kutokana na upana wa kikosi cha timu ya Yanga ambayo imeanza vizuri duru la kwanza kwa kufanikiwa kuvuna pointi 25, kumempa jeuri kocha Mkuu, Mwinyi Zahera kumwambia beki wake Juma Abdul ampe nafasi Paul Godfrey.


Zahera amesema kuwa amefanikiwa kumuangalia kwa ukaribu Paul na kumwamini hali ambayo imemfanya amwambie Abdul kuwa ampe nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza.


"Nimekaa na Abdul na kumwambia kwamba kwa sasa inabidi ampe nafasi mdogo wake ili aweze kujijenga zaidi ya hapo alipo kwa kuwa ndio anachipukia na nimemwani najua kama sitampa nafasi nitamharibu kisaikolojia ataniuliza kwa nini simpangi.


"Mchezo wa leo hatacheza hilo lipo wazi kwa kuwa ana adhabu ya kadi nyekundu ila akimaliza tu adhabu yake anarejea kikosi cha kwanza, bado ana nafasi kwa umri alionao na uwezo anaofanya anapaswa aongeze zaidi uzoefu," alisema Zahera.


Abdul amekuwa nje kutokana na kusumbuliwa na majeruhi nafasi yake imechukuliwa na Paul, ataukosa mchezo wa leo dhidi ya Ndanda nafasi yake itazibwa na Juma Abdul.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic