November 6, 2018


Na George Mganga

Mjumbe mpya wa bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mwina Kaduguda, amesema mikakati waliyonayo hivi sasa ni kuiondoa klabu hiyo kwenye hadhi ya ukongwe kuwa kubwa.

Kaduguda ameeleza hayo baada ya kuweza kuwa mmoja wa washindi baada ya uchaguzi mkuu wa klabu hiyo kufanyika juzi jijini Dar es Salaam.

Mwanachama huyo mkongwe maarufu kama Simba wa Yuda, amesema Simba ya sasa ni klabu kubwa maana haina sifa hizo na inastahili kuitwa kongwe pekee.

Ili kuuondoa ukwongwe huo, Kaduguda amesema hivi sasa watapambana kuhakikisha klabu inakuwa na hadhi ya kuitwa klabu kubwa baada ya kufanikisha kuwa mshindi.

Kwa kushirikiana na wenzake, Simba wa Yuda anaamini Simba itafika mbali na hii inachagizwa na mfumo mpya wa kisasa ambao inaelekea kuukamilisha kiuendeshwaji.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic