November 5, 2018


Kocha Mkuu wa timu Ndanda FC, Malale Hamsini amesema kuwa kikubwa kilichomsaidia kuweza kupata matokeo ni umakini wa wachezaji wake katika kufuata maelekezo na kujifunza kupitia makosa.

Malale amesema kuwa walikuwa na muda wa kujifunza hasa kwa wachezaji wake kutambua wachezaji wa timu ya Yanga hali iliyowasaidia waweze kuambulia pointi moja japo malengo yao ilikuwa ni kushinda.


"Tumefanikiwa kupata ushindi wa mapema ila mpira ni mchezo wa makosa hali ambayo ilitufanya nasi tukaruhusu kufungwa ila tumeyapokea matokeo tunajipanga kwa ajili ya michezo inayofuata," alisema.


Ndanda inakuwa timu ya pili kutoa sare na Yanga uwanja wa Taifa baada ya Simba kufanya hivyo pia, kwa matokeo hayo Ndanda wanakuwa na pointi 13.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic