November 30, 2018


Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefichua kuwa kilichomsaidia aweze kurejea Dar es Salaam na pointi sita ni morali ya wachezaji kujituma na kufuata maelekezo kwa umakini.


Yanga wamefanikiwa kuibuka na ushindi katika michezo yao 2 waliyocheza katika mkoa wa Shinyanga dhidi ya Mwadui na ule wa Kagera dhidi ya Kagera Sugar.


Zahera alisema kuwa wachezaji alionao wana uwezo mkubwa wa kufuata maelekezo pamoja na uzoefu kutokana na kufanya mazoezi kwenye viwanja vibovu.

"Wachezaji wangu wote wana uzoefu wa kucheza kwenye viwanja vibovu kwa kuwa hivyo ndivyo huwa tunafanyia mazoezi, haikuwa kazi kwao kupata matokeo kwenye michezo yetu.


"Sapoti kutoka kwa mashabiki wenye mapenzi ya kweli na timu kwa kuwa timu iliweza kusafiri kwa ndenge hali iliyofanya wachezaji kutokuwa na uchovu na kufanya kile ambacho niliwaelekeza," alisema Zahera.


Yanga wamecheza michezo 13 na kushinda michezo 11 huku wakitoa sare 2 na kufanya wawe na pointi 35 wakiwaacha Azam kwa pointi 2 na 8 kwa Simba ambao wapo nafasi ya 3.

2 COMMENTS:

  1. Wachezaji wa Yanga wanatakiwa kupewa pongezi kubwa sana..maana wapo katika kipindi ambacho hujui kuhusu kesho. Kinachosaidia ni uwezo wa kocha kuwaelesha wachezaji ili wawe watulivu. ..hiki ni kipindi cha mpito bila uvumilivu maisha yatakuwa magumu sana klabuni. Hongereni sana

    Lakini huwa najiuliza...ni kweli hakuna kiongozi mwenye fikra za kimaendeleo pale klabuni???Yanga ni Taasisi ambapo kiongozi anaweza kufanya matekelezo ya kifedha kupitia rasilimali zilizopo. Tuna vyanzo vingi vya kifedha na kama kiongozi wa Yanga huwezi kuniambia huwezi kuwapatia wachezaji mishahara kutokana na mapungufu ya fedha ndani ya Timu. Kama sportPesa anatoa zaidi ya Bilioni..sidhani kama tunashindwa kuwapa wachezaji mishahara yao.

    USHAURI KWA VIONGOZI WANAOGOMBEA HASA MWENYEKITI NA MAKAMU:::
    Hoja ya msingi...tuwape muda gani baada ya kuchaguliwa utatatua matatizo yaliyopo ndani ya Club????utasaidia vipi kwa muda mfupi kujenga uwanja wa Yanga kupitia wawekezaji????utaifanya vipi Yanga irudi kwenye njia yake hasa mashindano makubwa????utafanya vipi Yanga ijitegemee kifedha???utaijenga vipi Yanga yenye wachezaji wenye mikataba bora na iwe ya kibiashara????tuambie kwenye hilo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic