November 29, 2018


Baada ya Mbabane Swallows, kupokea kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa wawakilishi wa Tanzania Simba, kiungo wa Mbabane, Tony Tsabedze amesema kuwa walifungwa mabao mengi mepesi ambayo yamewagharimu.

Mbabane walipoteza mchezo wa kwanza mbele ya Simba uliochezwa uwanja wa Taifa hivyo ili waweze kusonga mbele wanatakiwa kuwafunga Simba zaidi ya mabao 3 katika mchezo wa marudio utakaochezwa Desemba 5.

"Tumefungwa ugenini hivyo nguvu zetu tunazielekeza kwenye mchezo wetu wa marudiano, tuna amini tutaweza kupindua meza kwa kuwa makosa mwalimu ameyaona na tutayafanyia kazi," alisema.

Simba walifanikiwa kufunga mabao hayo kupitia kwa nahodha John Bocco ambaye alifunga mabao 2 huku Meddie Kagere na Claytous Chama wakitupia moja moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic